Kibatui

Kibatui (pia Kibaha) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabatui kwenye kisiwa cha Sulawesi. Idadi ya wasemaji wa Kibatui imehesabiwa kuwa watu 2900. Kwa vile Wabatui wengi wameanza kuacha lugha yao, Kibatui imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibatui iko katika kundi la Kicelebiki.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search